9 Machi 2013 - 20:30

Ufaransa ambayo ipo kwenye operesheni ya kijeshi nchini Mali tangu mwezi Januari, hadi sasa imeshatuma askari elfu 4. Operesheni hiyo inayofanywa katika sehemu ya kaskazini nchini humo imekumbwa na wakati mgumu wa kushambuliwa tokea mwezi Machi, ambapo hadi sasa vifo vya askari wa Ufaransa vimeongezeka na kufikia vinne.

Mpango wa rais wa Ufaransa wa kuondoa jeshi mwezi Machi umeahirishwa hadi Aprili. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa, mapambano hayo makali dhidi ya jeshi la Ufaransa na ongezeko la vifo vya askari ni kutokana na kuwa hivi sasa jeshi la Ufaransa lipo katika eneo la mlima Ifo Las kaskazini mashariki mwa Mali ambalo ni ngome ya waislamu wenye siasa kali ambapo wana silaha na zana nyingi za kijeshi.

Wataalamu wa jeshi la Ufaransa wamesema, muda wa mapambano yanayofanywa na jeshi la Ufaransa utaweza kuongezwa hadi kufikia mwezi Julai.